Mashirika ya UM na serikali ya Uganda kuungana kwa ajili ya kilimo

13 Agosti 2015

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Serikali ya Uganda na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP, wamekubaliana kuanzisha mradi wa kuimarisha kilimo miongoni mwa wakimbizi na jamii zinazowahifadhi nchini humo, kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Katika mkataba wa makubaliano ambao umetiiwa saini na kamishina wa wakimbizi wa Uganda David Kazungu na wawakilishi wa UNHCR na WFP, watashirikina katika ujenzi wa miundombinu ya kijamii na kuanzisha matumizi ya mbinu za kisasa katika kilimo miongoni mwa mengine, kwenye kambi za Kyangwali na Rwamwanja.

Kaimu Mkurugenzi wa WFP Michael Dunford, amesema, lengo la mradi huu ni kupata wakimbizi na jamii zinazowahifadhi zilizoondokana na utegemezi, na kuboresha uhusiano wa kiuchumi na kijamii baina ya jamii hizo mbili.

Mradi huu unaotazamiwa kupanuliwa hadi katika nyanja za ufugaji na uvuvi, kwa sasa unawalenga watu 17,500.

Kamishina Kazungu ameonyesha matumaini kuwa kuwezesha jamii ya wakimbizi kutasaidia kukuza uchumi wa taifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter