Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna haja ya kukabiliana na hali, kuepusha janga la kibinadamu Somaliland: UM

Kuna haja ya kukabiliana na hali, kuepusha janga la kibinadamu Somaliland: UM

Naibu mpya wa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Peter de Clercq, amemaliza ziara yake ya kwanza ya Puntland na Somaliland.

Hii inakuja wakati Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na wadau wakikadiria kwamba kuna takriban wakimbizi wa ndani 220,000 Puntland na Somaliland, amao wana mahitaji ya dharura ya chakula, maji na makazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stéphane Dujarric amesema..

“Zaidi ya hayo zaidi ya watu 28,000 wamewasili nchini Somalia tangu Aprili, wakikimbia mzozo Yemen, wakiwemo raia wa Somalia na wakimbizi kutoka Yemen.”

Bwana de Clercq alitembelea pia vituo vya mapokezi katika miji ya pwani ya Berbera na Bosasso ambako alikutana na watu waliokuwa wakiwasili.

Kwa mantiki hiyo Naibu  Mwakilishi Maalum huyo amesisitiza umuhimu wa juhudi za haraka na pamoja na wadau wa kimataifa na mamlaka za kitaifa na za mitaa kwa ajili ya kuepusha janga la kibinadamu.