Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini Uganda, vijana waeleza kukosa fursa za ajira

Nchini Uganda, vijana waeleza kukosa fursa za ajira

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya vijana, Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa kushirikisha vijana kwenye sekta zote za jamii na kuwapa fursa za kushiriki pia kwenye uundwaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu vijana, Ahmad Alhendawi, kwenye ujumbe wake kwa siku hii amesema vijana wanaweza kubadilisha dunia ili iwe dunia inayostahili.

Barani Afrika hali ikoje? John Kibego kutoka Uganda amewauliza vijana kuhusu changamoto wanazokumbana nazo katika kutafuta ajira. Ungana naye kwenye makala hii