Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajumbe wa kimataifa wataka mazungumzo yarejelewe Burundi

Wajumbe wa kimataifa wataka mazungumzo yarejelewe Burundi

Wajumbe wa kimataifa wametoa wito leo kwa warundi wajiepushe na machafuko zaidi kwa kuonyesha uongozi na busara ili kuimaliza hali tete iliopo sasa kisiasa na kurejesha ustawi.Taarifa kamili na Ramadhani Kibuga.

(Taarifa ya Kibuga)

Miongoni mwa wajumbe waliotoa taarifa hiyo ya pamoja ni Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kwa ukanda wa Maziwa Makuu, Said Djinit, Mjumbe maalum wa Muungano wa Afrika, AU, Ibrahima Fall, wajumbe wa Marekani, Muungano wa Ulaya na Ubelgiji.

Wajumbe hao wamelaani mashambulizi ya hivi karibuni, yakiwemo mauaji ya Jeneral Adolphe Nshimirimana na mashambulizi dhidi ya mtetezi wa haki za binadamu, Pierre Claver Mbonimpa, na mwanahabari Esdras Ndikumana, na kuwapongeza wote wanaotoa wito wa kurejesha utulivu.

Ili kurejesha imani kufuatia miezi ya machafuko na uchaguzi uliozua utata, wajumbe hao wametoa wito kwa serikali ya Burundi ianze mazungumzo jumuishi ya kisiasa na wadau wa kisiasa, vikiwemo vyama vya upinzani na wakuu wa CNDD-FDD na mashirika ya kiraia.