Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya watu wa asili yamulikwa katika maadhimisho ya 2015

Afya ya watu wa asili yamulikwa katika maadhimisho ya 2015

Siku ya Watu wa Asili Duniani imeadhimishwa kwa mkutano maalum kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, maadhimisho yam waka huu yakimulika afya ya watu hao.

Azimio lililopitishwa na Baraza Kuu mnamo mwaka 2007 kuhusu haki za watu wa asili, limesaidia kuboresha maisha ya kundi hilo, lakini changamoto bado ni nyingi, ikiwemo kutopata huduma za kisasa za afya na kuathiriwa kwa maeneo wanakopata dawa za matibabu ya kiasili.

Katika mahojiano haya, Dkt. Priscilla Migiro, ambaye ni Mtaalam wa afya ya watoto, anaanza kwa kumweleza Joshua Mmali jinsi taaluma yake inavyoana na maadhimisho yam waka huu ya Siku ya Watu wa Asili.