Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ahukumiwa miaka 30 kwa kukosoa mfalme wa Thailand kwenye Facebook: UM yashtushwa

Ahukumiwa miaka 30 kwa kukosoa mfalme wa Thailand kwenye Facebook: UM yashtushwa

Ofisi ya Haki za Binadamu imesema imeshtushwa sana na vifungo vya miaka mingi vilivyotolewa hivi karibuni na Mahakama ya kijeshi nchini Thailand dhidi ya raia kadhaa kwa madai ya lese-majeste, yaani kumkosea mfalme na familia yake.

Tarehe 7, mwezi Agosti, Phongsak Sribunpeng alihukumiwa miaka 30 baada ya kuweka machapisho sita kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook ya kuhakiki familia ya mfalme. Watu wawili wengine wamehukumiwa miaka 25 na 28 kwa sababu hizo hizo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Ravina Shamdasani, amesema kwamba idadi ya watu waliohukumiwa au kufungwa kabla ya kuhukumiwa imeongezeka kutoka kwa watano kabla ya mapinduzi ya serikali hadi angalau 40 mwezi Mei mwaka huu, akitoa wito kwa serikali ya Thailand

“ Tunaomba watu wote waliofungwa kwa sababu wamejieleza huru waachiliwe mara moja. Pia tunaisihi serikali ya kijeshi kubadilisha sheria ya lese majeste ambayo ni pana na si dharihi, ili iwe sambamba na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.”