Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa UM aonya kuhusu kulazimu njaa kwa raia Yemen

Mtaalam wa UM aonya kuhusu kulazimu njaa kwa raia Yemen

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kupata chakula, Hilal Elver, ameonya leo kuwa taifa la Yemen limo katika hatari ya mzozo wa chakula, kufuatia mzozo  unaozidi kufukuta nchini humo. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Akieleza kusikitishwa na hali mbaya ya kibinadamu inayolikumba taifa hilo, Bi Elver amesema watu zaidi ya milioni 12.9 sasa hawapati chakula cha kutosha, wakiwemo milioni 6 wasio na uhakika wa chakula.

Mtaalam huyo amesema hali inayowakumba watoto inatisha zaidi, ripoti zikisema kwamba watoto laki nane na nusu nchini Yemen wanakabiliwa na utapiamlo uliokithiri. Idadi hiyo inahofiwa kupanda hadi milioni 1.2 katika majuma yajayo, iwapo mzozo utaendelea katika viwango vya sasa.

Aidha, ameonya kuwa kushambulia na kuzingira maeneo ya raia kunakozuia kufikisha bidhaa za ckakula kunasababisha njaa, na huenda kukawa ni uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.