Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya kigaidi Uturuki

Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya kigaidi Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea leo nchini Uturuki, ikiwemo dhidi ya vikosi vya usalama, kwenye mji mkuu wa Istanbul na pia kusini mashariki mwa nchi, na pia dhidi ya Ubalozi Mdogo wa Marekani nchini humo.

Kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake mjini New York, Bwana Ban amenukuliwa akieleza wasiwasi wake kuhusu ghasia hiyo.

Katibu Mkuu ametuma salamu zake za faraja kwa wahanga wa mashambulizi ya leo, pia kwa raia na serikali ya Uturuki.

Aidha amesema kuwa anatumai watekelezaji wa uhalifu huo watapelekwa mbele ya sheria.