Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumza na wanafunzi na mwalimu wa Palestina kwa skype

Ban azungumza na wanafunzi na mwalimu wa Palestina kwa skype

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekuwa na mazungumzo kwa njia ya skype na wanafunzi wawili wakimbizi wa Kipalestina pamoja na mwalimu wao kuhusu mustakabali wa elimu ya watoto wakimbizi walioko chini ya uangalizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina(UNRWA).

Katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu Ban amewatia moyo wanafunzi hao na mwalimu akiwaambia UM utafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa fedha zinapatikana ili warejee shuleni.

(SAUTI BAN)

‘‘Pamoja na Kamishna wa UNRWA Krähenbüh pia nimekuwaa nikizungumza na viongozi wa dunia kusaidia ili kuendelea na shule hizi za UNRWA.’’

Kwa upande wake mtoto Rua Nasira Abdulkidai mwenye umriwa miaka 11 ambaye shule yake iliharibiwa vibaya katika katika mapigano katia ya Israel na Palestina mwaka mmoja uliopita anamweleza Ban umuhimu wa elimu.

Akiongea kwa kiarabu na kutafsiriwa na mwalimu wake anasema.

(SAUTI RUA)

‘‘Elimu inanisaidia kuona mustakabali wa maisha yangu na kufanikiwa katika uwezo wangu.’’