Skip to main content

Mtalaam wa UM aonya Mauritania kuhusu haki za mashirika ya kiraia

Mtalaam wa UM aonya Mauritania kuhusu haki za mashirika ya kiraia

Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa  anayeshughulikia  haki za uhuru wa mikutano ya amani na mashirika, Maina Kiai ametoa wito kwa bunge la Mauritania  kutupilia mbali  mswada wa sheria  kuhusu mashirika uliodhinishwa na baraza la mawaziri  mwezi uliopita bila mashauriano. Ramadhani KIBUGA anaarifu zaidi.

(Taarifa ya Kibuga)

Bwana Kiai amesema ingawa anaunga mkono juhudi za Mauritania za kuimarisha na kufanyia marekebisho sheria zinahusu utendaji kazi wa mashirika ya kiraia, hata hivo anahofu kuwa mswada wa sheria jinsi ulivyo, unahatarisha uhuru na haki za msingi katika nchi hiyo hasa haki ya uhuru wa mikutano.

Aidha, Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ameonyesha wasiwasi wake kutokana na kutohusishwa mashirika ya kiraia katika maandalizi ya mswaada huo na swala zima la marekebisho ya rasimu ya sheria hiyo kuhusiana na mashirika, wakfu na mitando ya mashirika ikionekana kuwa hali ilivo mswada huo haukidhi viwango vya kimataifa.

Afisa huyo wa Umoja wa mataifa amesititiza kuwa ni lazima Serikali ya Mauritania izichukulie asasi za kiraia kama washirika muhimu katika mchakato huo wa mageuzi.

Bwana Kiai ameongeza kuwa sheria hiyo inaratibu mashirika katika utendaji wake kuomba ruhsa ya awali badala ya kuchukulia kuwa wajibu ni utaratibu wa kawaida wa kufahamisha tu ,na hii inaweza kuathiri kazi za mashirika hayo ya kiraia nchini humo Mauritania.

Mratibu huyo maalumu ameonya pia kwamba ikiwa sheria hiyo itaidhinishwa kwa hali ilivo, itatoa adhabu kali kwa mashirika na itapunguza wigo wa kujitanua kwa mashirika hayo katika nyanja yaa kazi za maendeleo.