Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo vya watoto wachanga yaongezeka Palestina: UNRWA

Idadi ya vifo vya watoto wachanga yaongezeka Palestina: UNRWA

Kiwango cha vifo vya watoto wachanga imeongezeka nchini Palestina kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo mitano limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Taarifa ya Amina.

(Taarifa ya Amina)

Kwa mujibu wa utafiti wa UNRWA sababu inayoweza kuchangia ongezeko la vifo hivyo katiika utafiti utafiri huo wa mwaka 2013 ni mgogoro ambapo maeneo waishio watoto hao yamekuwa magumu kuifikika na hivyo kukwama kwa huduma.

Utafiti unayonyesha kuwa idadi yawatoto wanaokufa kabla ya umri wa mwaka mmoja imeongezeka kwa asilimia 22.4 kwa watoto 1000 huko Gaza.

Takwimu pia zinaonyeha kuwa idadi ya watoto wachanga wanaozaliwa na kufa kabla ya majuma manne imeongezeka kutoka watoto 12 kati ya 1000 mwaka 2008, hadi asilimia 20.3 mwaka 2013.