UM watoa wito walindwe raia na uongezwe ufadhili wa misaada Yemen

10 Agosti 2015

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Yemen, Johannes Van Der Klaauw, amesema kuongezeka kwa mzozo nchini humo kuna madhara makubwa kwa raia, akitoa wito raia walindwe na uongezwe ufadhili wa kibinadamu.

Bwana van Der Klaauw ambaye amerejea kutoka ziarani mjini Sa’ada, amesema machafuko yamelazimu idadi kubwa ya watu kuhama makwao, huku miundo mbinu ya kiraia ikiharibiwa kwa makombora na mapigano.

Amesisitiza tena umuhimu wa pande kinzani kulinda maisha ya raia na mali zao, na kutaka miundombinu ya kiraia isilengwe katika mashambulizi ya angani, au kutumiwa kwa sababu za kijeshi.

Amesema wadau wa kibinadamu wanapaswa kuongeza jitihada zao ili kukidhi mahitaji makubwa ya watu milioni 21 wanaohitaji usaidizi wa kibinadamu kote nchini Yemen.

Ameongeza kuwa ufanisi wa jitihada hizo unategemea kuwepo ufadhili wa kutosha, na kutoa wito wahisani wachangie ombi la dola bilioni 1.6, ambazo zinahitajika kwa mwaka 2015.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter