Ban asikitishwa na kuuawa kwa walinda amani 5 wa Rwanda nchini CAR

Ban asikitishwa na kuuawa kwa walinda amani 5 wa Rwanda nchini CAR

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesikitishwa sana baada ya kupata taarifa ya kuuawa kwa walinda amani watano wenye uraia wa Rwanda waliokuwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wake imesema kwamba Katibu Mkuu ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga, pia raia na serikali ya Rwanda, huku akiwatakia nafuu waliojeruhiwa.

Halikadhalika taarifa hiyo imeeleza kwamba uchunguzi unaendelea ili kujua sababu za shambulio hilo ambapo walinda amani wengine wanane wamejeruhiwa.