Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afurahia kufanyika kwa uchaguzi nchini Haiti

Ban afurahia kufanyika kwa uchaguzi nchini Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amekaribisha utaratibu wa uchaguzi wa rais, bunge na serikail za mitaa utakaofanyika tarehe 9 Agosti nchini Haiti, akipongeza hasa jinsi raia wa Haiti waliovyozidi kumudu utaratibu huo.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, Katibu Mkuu amenukuliwa akisema uchaguzi huo ni hatua ya msingi kwa demokrasia nchini humo.

Aidha amesema uchaguzi huru, jumuishi na wa kuaminika ni msingi wa utulivu wa kudumu na demokrasia inayostawi.

Bwana Ban amevisihi vyama vya kisiasa, wagombea na wafuasi wao kuendesha kampeni kwa amani na kutatua shida zao kupitia majadiliano na mifumo ya sheria.

Amewaomba raia wote wa Haiti kushiriki kwenye uchaguzi, akiongeza kwamba Umoja wa Mataifa unaendelea kuuunga mkono utaratibu huo.