Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya unyonyeshaji yatia nanga

Wiki ya unyonyeshaji yatia nanga

Wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji iliyoanza rasmi mnamo Agosti mosi inatia nanga Agosti nane kwa hamasa kwa jumuiya ya kimataifa kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kuwanyonyesha watoto kwa afya zao. Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO na lile la kuhudumia watoto UNICEF, ambao ndiyo wenye dhamana katika maadhimisho ya juma hili kunyonyesha ndiyo njia bora ya kuwapatia watoto madini wanayohitaji na hivyo kushauri unyonyeshaji saa moja baada ya kuzaliwa kwa mtoto hadi mtoto atakapofikisha miezi sita. WHO inasema ziada ya lishe bora kwa mtoto yaweza kujumuishwa wakati unyonyeshaji ukiendelea hadi kipindi cha miaka miwili au zaidi. Maadhimisho haya yanajuimisha nchi zaidi ya 170 duniani zikiwemo nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambako kumekuwa na mawazo mgando kuwa kunyonyesha kunapoteza muonekano maridhawa kwa mwanamke. Hili limesababisha baadhi ya kina mama kutonyonyesha kabisa na hivyo kutafuta njia mbadala ambayo ni kumnyonyesha mtoto maziwa ya kopo. Kufahamu kwa undani  zaidi tuangalie hali ilivyo Afrika Mashariki.

(Studio Package)