Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtalaam wa Umoja wa Mataifa aomba wanaharakati wa haki walindwe Burundi

Mtalaam wa Umoja wa Mataifa aomba wanaharakati wa haki walindwe Burundi

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu wanaharakati wa haki za binadamu, Michel Forst, ameisihi leo serikali ya Burundi kulinda usalama wa wanaharakati wote nchini humo. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte

(Taarifa ya Priscilla)

Wito huo umetolewa leo baada ya shambulio dhidi ya mwanaharakati maarufu Pierre Clavier Mbonimpa ambaye mpaka sasa bado yuko hospitalini.

Bwana Forst amesema shambulio hilo ni dalili kwamba hali inazidi kuzorota nchini humo, akimulika ghasia inayotendeka na kundi la vijana lililo karibu na chama tawala, na kuongeza kwamba maisha ya wanaharakati wa haki yako hatarani.

Amesisitiza umuhimu wa kufanya uchunugzi juu ya shambulio hilo

(SAUTI FORST)

“ Tukiacha ukwepaji sheria utawale nchini humo dhidi ya watu kama Pierre Clavier Mbonimpa, ni dalili mbaya kwa watu wengine. Kujaribu kunyamazisha wanaharakati wa haki za binadamu na waandishi wa habari kwenye wakati huu ni jambo mbaya zaidi linaloweza kufanywa nchini humo.”