Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji Ugiriki sasa ni janga maradufu: UNHCR

Wahamiaji Ugiriki sasa ni janga maradufu: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR limesema idadi ya wakimbizi wanaowasili visiwani nchini Ugiriki sasa ni janga maradufu ambapo mwezi Julai pekee wakimbizi 50,000 waliwasili ikiwa ni ongezeko la 20,000 ikilinganishwa na mwezi Juni.

Hayo yamebainika baada ya ziara ya wakuu wa UNHCR wa ukanda wa Ulaya wanaoshughulikia pia dharura ambapo wamearifu kuwa wakimbizi na wahamiaji 124,000 wamewasili kwa njia ya bahari hiyo ikiwa ni takwimu ya kufikia Julai 31 pekee. Wamesema idadi kubwa ya wahamiaji ni kutoka nchi zenye migogoro mathalani Syria, Afghanistan na Iraq.

Vincent Cochetel ni mkurugenzi wa UNHCR kwa ukanda wa Ulaya

(SAUTI VINCENT)

"UNHCR inatoa wito kwa mamlaka ya ugiriki kuchukua hatua ya kuongoza na kuratibu,  tunawasiwasi ya kwamba hakuna shirika au mamlaka inayotaka kuchukua hatua ya uongozi, na hiyo inayapa shida kubwa mashirika ya kibinadamu kushiriki katika juhudi za kutoa msaada, kwa hiyo tunaziomba serikali kuu na za mitaa kutoa sehemu rasmi ambapo tunaweza kuwasaidia kukabiliana na hali hii na kuratibu msaada."