Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahudumu wa kibinadamu waanza kuwafikia waathiriwa wa mafuriko Myanmar - OCHA

Wahudumu wa kibinadamu waanza kuwafikia waathiriwa wa mafuriko Myanmar - OCHA

Wakati ripoti zinasema kuwa watu 88 tayari wameaga dunia kati ya zaidi ya 330,000 walioathiriwa na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi nchini Myanmar, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake wameongeza juhudi za kufikisha vifaa vya kuokoa maisha kwa waathiriwa.

Mratibu Mkaazi wa Maswala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Eamonn Murphy amesema, kwa bahati nzuri sasa wafanya kazi wa kutoa misaada wamepata uwezo wa kifikia maeneo yalioathiriwa, na wanafanya kila wawezalo kusaidia mamlaka za Myanmar kufikisha misaada kwa wote walio katika uhitaji.

Ameongezea kuwa timu za kutathimini misaada zinaungana mkono kushughulikia changamoto za kifedha mbele ya juhudi za kufikia maeneo yalioathiriwa zaidi ya Sagaing na Magway, na katika majimbo ya Rakhine na Chin.

Jens Laerke ni msemaji wa OCHA

Tuna hofu kwamba idadi hiyo itaendelea kuongezeka kadri  tunavyozidi kupata tathmini. Tunajua kwamba hali ya hewa imeimarika na maji yanaelekea kusini kwenye bahari sasa, lakini bado kuna wasiwasi kwamba mito itajaa na kufurika maeneo mengine zaidi.’