Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna uharibifu mkubwa mjini Sa’ada:Van Der Klaauw

Kuna uharibifu mkubwa mjini Sa’ada:Van Der Klaauw

Mratibu wa maswala ya kibinadamu kwa ajili ya Yemen, Johannes Van Der Klaauw ameshuhudia uharibifu mkubwa wa miundombinu ya raia katika miji ikiwemo katika masoko, benki na shule na kukutana na jamii za watu waliofurushwa makwao. Joseph Msami na taarifa kamili.

(TAARIFA YA MSAMI)

Katika ziara yake hiyo ya siku mbili ya ya mji wa Sa’ada Van Der Klaauw pia amekutana na mamlaka za mitaa na kutembelea  hospitali inayotoa huduma kwa ajili ya wahanga wa ukatili na watoto wanaoishi na ulemavu. Huku akiwapongeza watoa huduma hao kwa ujasiri wao na wadua wa kibinadamu na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambao wamesalia Sa’ada wakati huu wa mzozo.

Bwana Van Der Klaauw amehimiza umuhimu wa pande mbili kulinda maisha ya raia, akiongeza kwamba maeneo ya raia yanapaswa kulindwa dhidi ya mashambulizia ya anga na kuzingirwa na wakati huo huo hayapaswi kutumika kwa sababu za kivita.