Ni wakati mwafaka kwa mazungumzo ya amani Libya- UM

7 Agosti 2015

Umoja wa Mataifa umesema ni wakati mwafaka kuanza mazungumzo ya kupatia suluhu mzozo ulioko nchini Libya, mazungumzo hayo yakiwa yamepangwa kuanza tena kwenye Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

Bado haijulijkani na nani watakaoshiriki mazungumzo hayo ya amani, lakini watu wapatao 30 wanatarajiwa kuwasili mjini Geneva mnamo Jumatatu wiki ijayo kushiriki mazungumzo hayo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Ahmad Fawzi, amesema hajui ni kwa nini mpatanishi wa Umoja wa Mataifa katika mazungumzo hayo, Bernardinho Leon anaamini sasa ndio wakati mwafaka.

“Sijui ni kwa nini ameamua kuwa sasa ndio wakati mwafaka, lakini ni dhahiri kuwa anadhani ndivyo ilivyo. Asingetangaza hili bila kufikiria kuna sababu ya kutosha ya kuzileta pande kinzani hapa, mwedno wote huo kutoka kule hadi hapa Geneva.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter