Bei za vyakula chini kabisa tangu miaka sita

6 Agosti 2015

Bei za vyakula hasa maziwa na mafuta zimeendelea kupungua mwezi huu wa Julai na kufika kiwango cha chini kabisa kwa kipindi cha miaka sita.

Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO ambalo limesema bei za vyakula zimepungua kwa asilimia 19 tangu mwaka 2014.

Bidhaa zilizosababisha mwelekeo huo hasa ni vyakula vitokanavyo na maziwa, pamoja na mafuta, huku bei za sukari na nafaka zikiongezeka kwa takriban asilimia 2. Kwa upande wake bei ya nyama haikubadilika.

Kwenye taarifa yake FAO imesema sababu ya kupungua kwa bei hizo ni ongezeko la uzalishaji wa maziwa barani Ulaya na mafuta barani Amerika na Asia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter