Ban azungumza kwa simu na Rais Nkurunzinza wa Burundi

6 Agosti 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hapo jana amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ambapo Ban amesisitiza tamko lake la kulaani mauaji ya hivi karibuni ya Jenerali Adolphe Nshimirimana.

Taarifa ya ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu inasema pia Ban amelaani jaribio la mauaji ya mwanaharakati Clavier Mbonimpa nakueleza kusikitishwa kwake na matokeo ya kiusalama kufautaia matuko hayo  nchini Brundi.

Amemtaka Rais Nkurunziza kuanzisha tena majadilianoa ya kisiasa ambayo yameahirishwa tangu Julai 19.  Amehasisha mamalaka za Burundi kufanya kazi kwa karibu na jumuiya ya Afrika Mashariki katika juhudi za kusaka suluhu zinazoongozwa na Uganda.

Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa unaunag mkono juhudi za kusaka amani dhidi ya matatizo makubwa yanaoyoikabili Burundi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter