UNFPA yajikita kuwasaidia wanawake na wasichana Myanmar walioathirika na mafuriko

6 Agosti 2015

Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) limeingilia kati kusaidia serikali na mashirika ya kiraia katika kuwasaidia wathiriwa wa mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Myanmar, likiangazia zaidi maswala ya wanawake na wasichana. Taarifa kamili na John Kibego

(Taarifa ya Kibego)

Naibu Mwakilishi wa UNFPA nchini Myanmar, Kaori Ishikawa amesema, ni lazima wahakikishe usalama wa kila mama anayejifungua na mtoto wake na pia kulinda wanawake na wasichana dhidi ya ukatii wa kingono na aina nyingine za ukatili wa kijinsia.

Amesema mara nyingi wakati wa majanga asili, maswala nyeti ya wanawake na wasichana husahaulika na kutoa kipaumbele kwa mahitaji ya kawaida kama maji na chakula.

Miongoni mwa mengine, tayari UNFPA limetoa vifaa vya kujisafi vya akina mama wanaojifungua katika nchi hiyo, ambapo serikali inasema watu kadhaa wameaga dunia kati ya zaidi ya 200,000 walioathiriwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika majimbo kumi na mawili.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter