Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya haki za mtoto yalaani kuuawa kwa Shafqat Hussein Pakistan

Kamati ya haki za mtoto yalaani kuuawa kwa Shafqat Hussein Pakistan

Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za mtoto na Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili dhidi ya watoto, wamelaani kuuawa kwa Shafqat Hussein  nchini Pakistan, ambaye alikuwa na umri wa miaka 14 alipopatikana na hatia ya kosa la kuua.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Benyam Dawit Mezmur, amesema kuwa mauaji hayo yanasikitisha, na ni ukiukaji wa wajibu wa Pakistan kitaifa na kimataifa, huku kamati hiyo ikiitaka Pakistan irejeshe sitisho la kutekeleza hukumu ya kifo.

Mwakilishi maalum kuhusu ukatili dhidi ya watoto, Marta Santos Pais amesema mauaji hayo yanatia huzuni, na yanakiuka ahadi za Pakistan kuhusu haki za watoto.

Amesema Pakistan imeridhia mkataba kuhusu haki za mtoto na ule wa kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa, ambayo inaweka dhahiri kuwa hukumu ya kifo haipaswi kutolewa kwa mshtakiwa ambaye alikuwa chini ya umri wa miaka 18 wakati kosa lilipofanywa