Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya visa vya Ebola kupungua, bado kuna changamoto

Licha ya visa vya Ebola kupungua, bado kuna changamoto

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa kupungua kwa visa vya Ebola ilivyoonekana katika takwimu za hivi karibuni  kusichukuliwe kama ushahidi wa ushindi dhidi ya ugonjwa huo, ambao umewaua watu 11,281.Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Ikiwa imetangaza kisa kimoja tu kilichothibitishwa nchini Guinea na kingine kimoja nchini Sierra Leone katika ripoti yake ya kila wiki, WHO imesema bado kuna changamoto za kukabiliana nazo.

Shirika hilo la afya pia limesema jaribio lake la chanjo dhidi ya Ebola nchini Guinea limeonyesha ufanisi wa awali, na sasa itapanua utoaji chanjo hiyo.

Changamoto kubwa zaidi, kwa mujibu wa WHO, ni kumtambua kila mtu ambaye amekaribiana na mtu aliyeambukizwa kirusi cha Ebola.

Kwa sasa, WHO inafuatilia takriban watu 2000 nchini Guinea na Sierra Leone.