Skip to main content

Wasomali 116 warudi Mogadishu kutoka Kenya.

Wasomali 116 warudi Mogadishu kutoka Kenya.

Wakimbizi 116 wamewasili leo kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu, nchini Somalia, ikiwa ni mpango wa hiari wa kuwarejesha makwao wakimbizi wa Somalia waliosaka hifadhi nchini Kenya.

Wakimbizi hao walikuwa wametoka kambi ya Dadaab, ambayo ina wasomali 333,000.

Utaratibu huo wa kurejesha wakimbizi unatekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa ushirikiano na serikali za Kenya na Somalia kwa lengo la kuwarejesha Somalia wakimbizi 425,000 kwa kipindi cha miaka mitano.

UNCHR inawapatia wakimbizi hao msaada utakaowawezesha kuanzisha upya maisha yao nchini Somalia, huku hali ya usalama nchini humo ikiwa imeimarika kama  anavyoeleza Msemaji wa UNHCR nchini Kenya Emmanuel Nyabera.

(Sauti ya Emmanuel. )