Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni vigumu kuongoza dunia inayowayawaya: Rais Baraza la Usalama

Ni vigumu kuongoza dunia inayowayawaya: Rais Baraza la Usalama

Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi Agosti kutoka Nigeria, Balozi U. Joy Ogwu, amewaambia waandishi wa habari mjini New York hii leo kuwa dunia imejaa machafuko na hivyo ni changamoto kubwa kutekeleza mipango ya maendeleo katika sayari ambayo moto unafuka sahemu nyingi.

Katika mkutano na waandishi wa habari wa kueleza mpango wa baraza hilo kwa mwezi huu balozi Ogwu amesema anaongoza chombo hicho katika wakati mgumu wa machafuko kote duniani.

(SAUTI OGWU)

‘‘Watu wengi wamepoteza makazi yao na huenda wasirudi kamwe, watoto inabidi wasome katika utulivu, tunaweza vipi kujenga upya dunia yetu? Kwa upande mwingine tuna dhamira ya malengo ya maendeleo endelevu, baada ya yale ya milenia MDGS.’’

Hata hivyo amesema ni muhimu jumuiya kimataifa itambue kuwa kila mtu ni mdau katika kuhakikisha amani na uslama huku msukumo wa maendeleo ukitakiwa kutokuachwa nyuma.