Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya nusu ya watu CAR wanahitaji msaada : OCHA

Zaidi ya nusu ya watu CAR wanahitaji msaada : OCHA

Zaidi ya watu milioni 2.7 kati ya idadi ya watu milioni 4.6 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, wanahitaji malazi, chakula, huduma msingi za afya, ulinzi, maji na huduma za kujisafi na msaada wa mahitaji mengine  ya kibinadamu imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.

Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Bangui mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini humo Aurélien Agbénonci, amesema takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 368,000 ni wakimbizi wa ndani nchini humo, huku wengine takribani 460,000 wakiwa wakimbizi katika nchi jirani. Idadi hii inatokana na machafuko yanayoendelea nchini CAR.

Amesisitiza kuwa hali ya usalama nchini humo inasalia tete kutokana na ukatili na mapigano kati ya vikundi kinzani vyenye silaha .

Bwana Agbénonci hata hivyo amesema kuwa baadhi ya wakimbizi wa ndani wamerejea kwa hiari  katika ameneo yao baada ya kurejea kwa amani huku pia mchakato wa kurejea kwa hiari kwa wakimbizi wa ndani kutoka kambi iitwayo M'Poko mjini Bangui unaendelea. Hadi tarehe  26 mulai wakimbizi zaidi ya 4000 wameshajisajili kuondoak kwa hiari .