Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha wanawake wanapata fursa kuwa mama:ILO

Kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha wanawake wanapata fursa kuwa mama:ILO

Idadi ya wanawake wanaofanya kazi inaendelea kuongezeka, na hivyo ni muhimu kufanya maamuzi ambayo yatawezesha akina mama kutekeleza wajibu wao kama mama na kuendeleza shughuli zao za kikazi ili kumudu mahitaji yao. Hiyo ni kauli ya Susan Maybud, mtaalam wa masuala ya kijinsia katika Shirika la Kazi Ulimwenguini, ILO, wakati wiki ya unyonyeshaji watoto ikiendelea.  Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Katika mahojiano na Radio ya Umoja wa Mataifa, Bi Maybud amesema kwamba jukumu la kuhakikisha kwamba wanawake wanapata fursa ya kuwa mama ni la kila mtu.

Kwa mantiki hiyo, amesema kwamba ILO ina mkataba wa kulinda akina mama na kuhakikisha kwamba wanapata angalau siku 14 za mapumziko baada ya kujifungua, na mazingira ya kumwezesha mama  kunyonyesha mtoto baada ya kurudi kazini.

Hata hivyo Bi. Maybud ametoa angalizo…

Baada ya kuweka mikataba na kuweka sheria, suala kuu ni utekelezaji , kwa sababu si kwamba kila mtu atafuata sheria. Lakini kizuizi ni zaidi ya unyonyeshaji, ni ubaguzi dhidi ya wanawake wanaoajiriwa na wale wanaotaka kulinda ajira zao. Kuna waajiri ambao wanawafuta wanawake kazi  kwa sababu ni wajawazito au pindi baada ya kujifungua na wanachofanya ni kwamba wanapunguza idadi ya watu wanoajiriwa.”