Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yakaribisha mpango wa Obama wa nishati safi

UNEP yakaribisha mpango wa Obama wa nishati safi

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, Achim Steiner, amekaribisha mpango wa Rais Barack Obama wa Marekani wa nishati isiyochafua mazingira, akiutaja kama utashi wa kupunguza uzalishaji wa gesi ya mkaa na kuongeza nishati huishi kama vile ile itokanayo na upepo.

Bwana Steiner amesema mpango huo uliotangazwa hapo jana ni ishara muhimu kutoka kwa Marekani, miezi michache kabla ya mazungumzo ya Paris kuhusu tabianchi, COP21.

Ameongeza kuwa mpango huo unaongeza msukumo katika kukaribia COP21, akitarajia kuwa uongozi wa Rais Obama na ule wa viongozi wengine utasaidia kufikia mkataba wa kudumu baina ya nchi zote mwezi Disemba.

Amesema mabadiliko ya tabianchi ndilo suala muhimu zaidi la nyakati zetu, na kwamba tuna wajibu wa kuchukua hatua mathubuti kwa ajili ya vizazi vijavyo.