Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya unyonyeshaji watoto yang'oa nanga

Wiki ya unyonyeshaji watoto yang'oa nanga

Wiki ya unyonyeshaji watoto duniani ikiwa imeanza Agosti mosi hadi saba, nchi zaidi ya 170 zinaadhimisha juma hilo kwa wito kutoka shirika la afya ulimweguni WHO likihimiza unyonyeshaji watoto na kuimarisha afya za watoto.

WHO inasema kunyonyesha ndiyo njia bora ya kuwapatia watoto madini wanayohitaji na hivyo kushauri unyonyeshaji saa moja baada ya kuzaliwa kwa mtoto hadi mtoto atakapofikisha miezi sita.

Shirika hilo la afya ulimwenguni limesema ziada ya lishe bora kwa mtoto yaweza kujumuishwa wakati unyonyeshaji ukiendelea hadi kipindi cha miaka miwili au zaidi.

Gladys Mugambi ni msimamizi wa lishe bora, wizara ya Afya Kenya na anaeleza mikakati ya nchi hiyo katika kuhakikisha unyonyeshaji kwa watoto.

(SAUTI MUGAMBI)