Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani mauaji ya mtoto wa Kipalestina kwa moto

Baraza la Usalama lalaani mauaji ya mtoto wa Kipalestina kwa moto

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo wameeleza kusikitishwa sana na kulaani vikali shambulizi la kigaidi lililofanywa katika kijiji cha Duma, karibu na Nablus kwenye Ukingo wa Magharibi, ambalo lilimuua mtoto wa Kipalestina na kuwajeruhi watu wa familia yake.

Katika taarifa yao ya Ijumaa usiku, Wajumbe wa Baraza la Usalama wamepeleka rambirambi zao kwa familia ya mtoto huyon na mamlaka za Palestina na watu wake.Wamesisitiza haja ya kuwafikisha washukiwa wa uhalifu huo mbele ya sharia.

Wamelaani pia aina zote zsa vitendo kama hivyo vya ukatili, ambavyo vimeathiri watu wa Palestina na Israel, wakielezea kutiwa wasiwasi na kuongezeka hali tete, na kutioa wito utulivu urejeshwe mara moja.

Wajumbe hao pia wamesisitiza umuhimu wa taarifa zote za kulaani shambulio hilo na vitendo vyote vya kikatili, na kuhimiza pande zote kufanya jitihada za kupunguza utata, kupinga ghasia, kujiepusha na uchochezi na kutafuta njia ya kuelekea Amani