Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UNHCR Angelina Jolie azuru wakimbizi Kachin, Myanmar

Mjumbe wa UNHCR Angelina Jolie azuru wakimbizi Kachin, Myanmar

Mjumbe maalum wa UNHCR, Angelina Jolie Pitt, amesadfiri kwenda mji wa Myitkyina katika jimbo la Kachin nchini Myanmar, ambako zaidi ya watu 100,000 wamelazimika kuhama tangu makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya vikosi vya usalama vya Myanmar na makundi ya kikabila yaliyojihami yavunjike mnamo mwaka 2011.

Bi Jolie amekutana na kuzungumza na familia za wakimbizi, na kusikiliza hadithi za changamoto zinazohusiana na upatikanaji wa huduma za msingi, hususan huduma za afya.

Ajuza mmoja mwenye umri wa miaka 90 ameelezea jinsi alivyolazimika kuhama mara nyingi katika maisha yake, akiwa amelazimika kuhama takriban mara 10 tangu miaka ya 60 na mwaka 2012.

Bi Jolie amesisitiza umuhimu wa kufikisha misaada ya kibinadamu kwa familia zilizofurushwa makwao. Hakuna wahudumu wa kibinadamu wa kitaifa au wa kimataifa walioweza kulifikia eneo hilo la mzozo tangu maachfuko yalipoanza mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.