Skip to main content

Makala yenye kuangazia siku ya urafiki duniani

Makala yenye kuangazia siku ya urafiki duniani

Tarehe 30 Julai, jamii ya kimataifa imeadhimisha siku ya urafiki duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisema urafiki hujenga daraja baina ya watu, na hivyo huchochea amani duniani. Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo, Bwana Ban amesema urafiki ni muhimu sana kwenye dunia ya leo inayokumbwa na ubaguzi, ukatili na mizozo inayoathiri mamilioni ya watu.

Bwana Ban amesema tunapaswa kukuza mawasiliano baina ya binadamu duniani ili kuheshimiana, kuelewana na kutokomeza chuki zinazosababisha uharibifu mwingi duniani. Nchini Burundi, sintofahamu na ukosefu wa uaminifu baina ya makabila ya watutsi na wahutu ulisababisha mauaji na kuibuka kwa mzozo wa kisiasa kwenye miaka ya 90 ulioendelea hadi makubaliano ya Arusha ya Agosti, 28, 2000. Kwa mtazamo wa warundi wengi uelewano na maridhiano baina ya wahutu na watutsi ni msingi wa amani ya kudumu nchini humo.

Mwenzetu Ramadhani Kibuga amefanya utafiti kuhusu hilo mitaani Bujumbura, nchini Burundi. Ungana naye kwenye makala hii…