Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji haramu wa binadamu tatizo Afrika Mashariki, juhudi zahitajika: Niyonzima

Usafirishaji haramu wa binadamu tatizo Afrika Mashariki, juhudi zahitajika: Niyonzima

Wanawake na watoto ni waathirika wakubwa katika usafirishaji haramu wa binadamu Afrika Mashariki amesema Mkurugenzi wa taasisi inayojihusisha na kuwakwamua wanawake na watoto katika unyanyasaji, ijulikanayo kama Connected hearts Bi Nelly Niyonzima.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii kuhusu siku ya kiamataifa ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu iliyoadhimishwa jana , Bi Niyonzima  anasema hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa na wadau kukomesha hali hiyo.

(SAUTI)

Amesema maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu ni muhimu katika kuchochea nguvu ya pamoja ya kukabiliana na vitendo hivyo.