Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji watu washamiri Tanzania: IOM

Usafirishaji watu washamiri Tanzania: IOM

Nchini Tanzania nako ofisi ya Umoja wa Mataifa imeadhimisha siku ya kupinga usafrisishaji haramu wa binadamu ambapo imeelezwa kuwa biashara hiyo haramu imenawiri sasa nchini humo ikifanywa na mawakala bubu.

Akiongea wakati wa maadhimisho hayo yaliyowaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwamo vyombo vya sheria afisa wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM Tanzania, Susan Bipa amesema wasichana ndio wanaoathirika zaidi kwa kusafirishwa mijini kwa kigezo cha ajira na chamgamoto katika kukabiliana na biashara hiyo ni..

(SAUTI)

Kwa mujibu wa IOM Iringa, Dodoma, Singida na Mbeya ni mikoa inayoongoza kwa usafirishaji haramu wa binadamu.