Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubakaji Zanzibar: “yule yule aliyenifanya tendo, kafungwa, kisha kaachiliwa”

Ubakaji Zanzibar: “yule yule aliyenifanya tendo, kafungwa, kisha kaachiliwa”

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF linakadiria kuwa mtoto wa kike mmoja kati ya ishirini anatendewa ukatili wa kingono kisiwani Zanzibar kabla ya kufikisha miaka 18, lakini wengi wao wanashindwa kuripoti kesi hizo polisi, na bado ukwepaji sheria ni changamoto.

Kupitia ushaidi wa mhanga mmoja kutoka Zanzibar, UNICEF inaonyesha umuhimu wa kuimarisha utendaji kazi wa polisi katika swala hilo.

Kulikoni? Priscilla Lecomte anayo zaidi.