Urafiki wa kweli ni kusaidiana :Waganda

30 Julai 2015

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Urafiki, inayotumiwa na Umoja wa Mataifa kujenga urafiki na kuunganisha jamii kwa ajili ya amani na ustawi, nchini Uganda raia wa nchi hiyo wanaeleza kwao urafiki una maana gani .

Katika mahojiano na mwandishi wetu John Kibego kutoka Hoima nchini humo, wahojiwa hao wanaeleza mengi lakini kubwa zaidi kwao urafiki ni kusaidiana nyakati zote.

(SAUTI MAHOJIANO)

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii tibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-moon amesema dhana hii ambayo ni wazo la shujaa mwenye maono laweza kujenga madaraja miongoni mwa watu na kuchochea amani duniani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter