Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji wa uchumi wapungua barani Amerika Kusini 2015: ripoti ya UM

Ukuaji wa uchumi wapungua barani Amerika Kusini 2015: ripoti ya UM

Ukuaji wa uchumi unatarajiwa kupungua kwenye bara la Amerika Kusini, Amerika ya Kati na Karibia mwaka 2015, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo.

Kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2015 kinatarajiwa kufika asilimia 0.5 kwenye ukanda huo, tofauti kati ya nchi zikiwa nyingi, imesema ripoti hiyo. Mathalan uchumi wa Panama utakua kwa asilimia 6 wakati ambapo uchumi wa Venezuela na Brazil ukitarajiwa kupungua.

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ukanda wa Amerika Kusini, ya Kati na Karibia ECLAC, Alicia Barcena, amesema mwelekeo huo wa kupunguka kwa ukuaji wa uchumi umesababishwa na kupunguka kwa kiwango cha uwekezaji, pia na matokeo ya kupunguka kwa ukuaji wa uchumi kwenye nchi nyingine duniani, hususan China.

ECLAC imesema uwekezaji zaidi unahitajika ili kuimairisha ufanisi wa uzalishaji na ukuaji wa uchumi.