UNESCO na Iraq zazindua mradi wa kutunza eneo la Urithi wa Dunia la Samara

29 Julai 2015

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, na serikali ya Iraq, leo zimetia saini makubaliano ya kutunza na kudhibiti eneo la Urithi wa Dunia la mji wa akiolojia wa Samara, ambayo yataanzisha ukarabati wa Msikiti Mkuu na Mnara wa Al-Malwiyah.

Eneo hilo limekuwa kwenye orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia ulio Hatarini tangu mwaka 2007.

Makubaliano hayo yamesainiwa kwenye makao makuu ya UNESCO mjini Paris na Ahmed Abdullah Abed Abed, Waziri wa taifa wa Masuala ya Majimbo na Ubunge nchini Iraq, Ammar Hikmeit Abdulhasan, Naibu Gavana wa Salah-Al-Din na Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO.

Katika hafla hiyo ya utiaji saini, waliozungumza wamesisitiza kuwa makubaliano hayo yanaonyesha utashi mkubwa wa kulinda urithi wa kitamaduni wa Iraq, ambao unakabiliwa na tishio lisilo ambalo halijawahi kuwepo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter