Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi Burundi haukuwa huru: UM

Uchaguzi Burundi haukuwa huru: UM

Baraza la Usalama limekuwa na mjadala wa faragha kuhusu uchaguzi uliofanyika Burundi tarehe 21 Julai, ambapo kikao hicho kimepokea taarifa kutoka Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kufauatilia uchaguzi nchini Burundi(MENUB). Taarifa kamili na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA)

Baada ya mkutano huo, wa faragha Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu, mwakilishi wa kudumu wa New Zealand kwenye Umoja wa Mataifa, Jacobus van Bohemen ameongea na waandishi wa habari  na kuwaleza kile kilichojiri.

Amesema Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa maswala ya kisiasa, Taye Brook Zerihoun pamoja naNaibu mkuu wa MENUB  Issaka Souna, wamewaelezea wanachama wa Baraza la Usalama kuhusu matokeo ya uchaguzi Burundi akisema kuwa mazingira ya uchguzi huo hayakuwa mazuri hivyo uchaguzi haukuw ahuru na jumuishi.

Amesema hitimisho la ripoti hiyo linafanana na la jumuiya ya Afrika Mashariki na akasema baraza limeshauriwa.

(SAUTI JACOBOUS)

“Msaidizi wa Katibu Mkuu Zerihoun amesisitiza umuhimu kwa Baraza la Usalama kuendelea kuiunga mkono Jumuiya ya Afrika Mashariki na utaratibu wa mazungumzo unaoongozwa na Uganda na kwa wadau wote kushiriki mazungumzo hayo. Wanachama wengi wa Baraza hilo wamependelea mazungumzo yaanze tena haraka na kwa njia jumuishi na wadau wote. Baraza pia limekariri msimamo