Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA, AKF kuinua elimu ya watoto Gaza

UNRWA, AKF kuinua elimu ya watoto Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina(UNRWA) limetiliana saini mkataba wa masaidiano na taaisisi ya kiisilam iitwayo Al-Khair (AKF) ya nchini Uingereza kwa ajili ya kusaidia elimu kwa watoto waliozingirwa katika ukanda wa Gaza.Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Taarifa ya UNRWA imesema kuwa AKF itaipatia shirika hilo dola za kimarekani zaidi ya 700,000 ikiwa ni sehemu ya mpango huo wa elimu ambapo utahusisha ujenzi wa shule sambamba na kampeni ya UNRWA ya elimu iliyozinduliwa hivi karibuni iitwayo #SOS4Gaza campaign.

Shirika hilo linasema ushirikiano katia yake na taasissi ya AKF ni matokeo ya kuwa na lengo moja la la kuondoa mateso katika maeneo ya dunia ambayo yamekosa fursa.

Mwenyekiti wa AKF Imam Qasim Rashid Ahmad amenukuliwa akisema kuwa ushitrikiano wa taasisi hiyo na UNRWA ni sehemu muhimu ya malengo yao ya kusongesha juhudi za kusaidia wahitaji husuani Mashariki ya Kati.