Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN Women yazindua ripoti kuhusu maendeleo ya wanawake duniani 2015-2016

UN Women yazindua ripoti kuhusu maendeleo ya wanawake duniani 2015-2016

Ripoti mpya imezinduliwa leo nchini Pakistan na Shirika la masuala ya Wanawake katika Umoja wa Mataifa, UN Women, ikibainisha ajenda-sera mbadala ya kubadili chumi za nchi mbali mbali na kufanya ndoto ya usawa wa jinsia itimie. Taarifa kamili na John Kibego.

Taarifa ya John Kibego

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kuna idadi kubwa sana sasa ya wanawake waliopata elimu, ikiwemo nchini Pakistan ambako kuna ushahidi kuwa wasichana wanafanya vizuri zaidi kuliko wavulana katika fani za udaktari, hisabati na kusoma.

Ripoti inasema licha ya hayo, kinaya ni kwamba wanawake bado wanahangaika kupata ajira, na kwamba sera zilizopo sasa kiuchumi na kijamii zinawafeli wanawake katika nchi tajiri kama ilivyo katika nchi maskini.

Ikimulika masuala ya haki za binadamu na utungaji sera za kiuchumi, ripoti inatoa wito wa kufanyia mabadiliko ajenda-sera ya dunia, ili kubadilisha uchumi na kuhakikisha haki za wanawake na usawa wa jinsia.