Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yapinga hukumu za maofisa Libya akiwemo mtoto wa Qadhafi

UNSMIL yapinga hukumu za maofisa Libya akiwemo mtoto wa Qadhafi

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL umeeleza wasiwasi wake kuhusu hukumu za maofisa 37 wa rais wa zamani wa Lybia Kanali Muammar Qadhafi akiwamo mtoto wake zilizotangazwa leo. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(TAARIFA YA MSAMI)

Taarifa iliyotolewa leo na UNSMIL imesema kesi za maofisa hao hazikuwa sawa kulingana na viwango vya kimataifa mathalani mtoto wa Qadhafi, Said Al-Islam Qadhafi ambaye amehukumiwa kunyongwa bila kupelekwa mahakamani kufautia serikali ya Libya kukataa kusikiliza amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC ya kumpeleka The Hague ili ahukumiwe huko.

Waziri mkuu wa zamani wa Lybia na watu nane wengine wamehukumiwa kifo, huku wengine nane wakihukumiwa kifungo cha maisha wengine vifungo vya miaka kadhaa ambapo UNSMIL imekariri msimamo wa Umoja wa Mataifa wa kupinga hukumu za kifo.

Halikadhalika changamoto zingine zilizokumba kesi hiyo zimetajwa na UNSMIL, ikiwa ni washtakiwa wengine kukosa mawakili, pia ukosefu wa ushahidi na mashahidi.

Hatimaye UNSMIL imeisihi serikali ya Libya kubadilisha sheria yake ili kuwezesha wahukumiwa hao kukataa rufaa.