UNRWA yajadili ukata unaolikumba shirika

UNRWA yajadili ukata unaolikumba shirika

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina(UNRWA) inaendesha vikao vya tume ya ushauri kujadili ukata wa fedha unaolikumba shirika hilo ambao umeelezwa kwua ni mkubwa kuliko wakati wowote.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, tume hiyo itajadili hatari inayoongezeka ya UNRWA ya kuchelewa kuanza kwa masomo kwa shule 700 na kuwaathiri watnusu milioni ikiwa hitaji la dola milioni 101 halitatolewa kabla ya mwaka wa masomo kuanza. Mkutano huo unafanyia nchini Jordan na kuwakutansiha pamoja wahisani wa shirika hilo na serikali wenyeji.

Kamishna Mkuu wa UNRWA Pierre Krähenbühl. Amenukuliwa akisema kuwa kuchelewa huko kutaongeza kukata tamaa kwa mamaia kwa amelfu ya wavulana na wasichana wenye nia thabiti ya kujiendeleza kielimu na kuongeza kuwa elimu ndiyo utambulisho na utu wa wakimbizi wa Kipalestina .