Mpango wa kukomesha umaskini wapitishwa na baraza kuu

27 Julai 2015

Mpango mpya wa kukomesha umaskini umepitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jumatatu hii ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema ajenda ya mpango ya Addis Ababa inatoa mkakati mpya wa ufadhili endelevu kwa maendeleo.

Ajenda hii ni matokeo ya waraka wa kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo, mkutano wa siku nne uliomalizika mapema mwezi huu.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepitisha ajenda hiyo ambapo Katibu Mkuu amesema unatoa mwongozo wa utekelezaji kwa wadau wote.

(SAUTI BAN)

"Inatoa motisha kwa wawekezaji katika maeneo yenya mahitaji kimataifa, kuwezesha mtiririko wa fedha na sera za kiuchumi na kipaumbele cha mazingira."

Ban amesema ajenda imeweka msingi imara katika kusukuma mbele malengo ya maendeleo endelevu au SDGS ambayo yanatarajiwa kupitishwa na nchi wanachama mwezi Septemba mwaka huu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud