Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wafanyika Madrid kujadili tishio la wapiganaji wanaovuka mipaka

Mkutano wafanyika Madrid kujadili tishio la wapiganaji wanaovuka mipaka

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi inakutana leo mjini Madrid Uhispania kujadili jinsi ya kusimamisha wapiganaji wanaovuka mipaka kwa ajili ya kujiunga na vikundi vya kigaidi.

Lengo la mkutano huo ni kuunda mikakati ya kuzisaidia nchi wanachama kukabiliana na tishio hilo.

Akizungumza na redio ya Umoja wa Mataifa kabla ya mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kamati hiyo, Jean-Paul Laborde, amesema mkakati huo unapaswa kufanywa kwa ngazi ya kimataifa ili kupambana na vikundi vya kigaidi kwa sababu:

“ Mashirika hayo yanachukua hatua mbio sana, kwa hiyo, sisi hatuna kasi ya kutosha kupambana nao. Pia jitihada zetu za kubaliana na maswala hayo kwa ngazi ya kitaifa hazitafanikiwa.”

Kwa mujibu wa kamati hiyo ya kupambana na ugaidi, ni zaidi ya watu 25,000 waliosafiri Syria na Iraq kutoka nchi 100 tofauti, ili kujiunga na vikundi vya kigaidi au venye itikadi kali.