Kay alaani shambulio la kigaidi mjini Mogadishu

27 Julai 2015

Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia Nicholas Kay  amelaani shambulio la Kigaidi linalodaiwa kutekelezwa na Al Shabaab  lililosababisha watu kadhaa kuuwawa  na wengine kujeruhiwa nchini humo. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Akilaani vikalio shambulio hilo lilkitokea kwenye Hoteli ya Jazeera katika mji mkuu wa Somalai Mogadishu, Bwana Nicholas Kay amesema, wauaji hao wanapaswa kuwajibishwa kisheria haraka iwezekanavyo.

Ametuma salamu za rambiramabi kwa serikali ya Somalia, familia na marafiki za waliouwauwa wakiwemo Mbunge  Abdulahi Hussein Mohamud na Sai'd Ali Saleh, maafisa wa serikali waliouwauwa kwa kupigwa risasi.

Bwana Kay amewapongeza wanausalama wa Somalia kwa kuitikia shambulio hilo na kusisitiza kuwa Umoja wa Mataifa na wadau wake watandelea na juhudi zao kutimiza ndoto ya Wasomali ya kupata utulivu katika siku za baadaye.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter