Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaiomba Ugiriki kujitahidi zaidi kwa ajili ya wahamiaji

UNHCR yaiomba Ugiriki kujitahidi zaidi kwa ajili ya wahamiaji

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia wakimbizi UNHCR limeiomba serikali ya Ugiriki kujitahidi zaidi ili kusaidia wahamiaji wanaowasili nchini humo, licha ya mzozo wa kiuchumi unaokumba nchi hiyo.

Kwa mujibu wa UNHCR, zaidi ya wahamiaji 100,000, wengi wao wakitoka Syria, wamefika kwenye visiwa vidogo vya Ugiriki wakivuka bahari ya Mediteranea kutoka Uturuki, UNHCR ikiongeza kwamba visiwa hivyo havina uwezo wa kuwapokea, licha ya jitihada za watu wa kujitolea na hata watalii.

Msemaji wa UNHCR William Spindler amewaambia waandishi wa habari leo mjini Geneva kuwa Ugiriki inahitaji msaada wa Muungano wa Ulaya, kutokana na changamoto za kiuchumi zinazokumba Ugiriki siku hizi.

Ameeleza kwamba tatizo la uhamiaji linahusu Ulaya nzima, kwani asilimia 95 ya wahamiaji hawabaki Ugiriki lakini wanahamia kwenye nchi nyingine za Ulaya. Hata hivyo, wanahitaji huduma za maji, chakula na makazi wanapowasili.