Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Flavia Pansieri anajiuzulu kwa ugonjwa si vinginevyo: Zeid

Flavia Pansieri anajiuzulu kwa ugonjwa si vinginevyo: Zeid

Kamishana Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein ametoa ufafanuzi kuhusu hatua ya kujiuzulu  kwa  Naibu Kamsihan Mkuu  wa haki za binadamu  Flavia Pansieri  na kusema kuwa ni kutokana na magonjwa na si vinginevyo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva Kamishina Zeid amesema kumekuwa na taarifa zisizio na ukweli kuwa kujiuzulu kwa Bi Pansieri kulitokana na uchunguzi unaoendelea kuhusu tuhuma za ubakaji wa watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR unaodaiwa kufanywa na wanajeshi wa Ufaransa.

Amesema kuwa  kiongozi huyo amezorota kiafya  hivi karibuni alifanyiwa upasuaji lakini hata hivyo akaonyesha adhma ya kumalizai majukumu hadi pale mteule wake atakapotangazwa licha ya kwamba haina uhakika ikiwa jicho lake litaona tena vyema baada ya kuathiriwa.

Kamishna Zeid pia ameasema kuwa Pansieri amepatwa na magonjwa mara tatu mwaka huu na kulazwa katika chumba cha dharura mara mbili ikiwa ni Januari na mwanzoni mwa mwezi Julai.